pmbet

Je, wajua kupenda sana ngono ni ugonjwa wa akili?

Eric Buyanza

January 15, 2024
Share :

Hivyo msomaji ni vyema leo ukatambua kuwa, kupenda sana kufanya ngono kupita kiasi ni tatizo la kiakili na ni vyema likachukuliwa kwa uzito kama yanavyotiliwa maanani matatizo mengine ya kiafya.
 

Tatizo hilo kitaalamu linajulikana kama (Nymphomania) kwa wanawake lakini pia kwa wanaume linajulikana kama (Satyriasis) lakini kwa ujumla ni ile hali ya mtu kuwa na tamaa ya kushiriki tendo kupita kiasi.
 

Tatizo hili linakuja kwa sura mbalimbali pasipo mtu kujijua, lakini baadhi ya dalili kuu za tatizo hili ni pamoja na kupenda sana tabia ya kujichua, kuwa na idadi kubwa ya watu unaofanya nao ngono, kupenda sana kuangalia video za ngono, kupendelea kufanya ngono pasipo kutumia kinga, kupendelea kuwa karibu na sehemu ambayo kuna wafanya biashara ya ngono kutokana na ukweli kuwa utaweza kufanya ngono kirahisi na kwa maelewano madogo na pia kujikuta wakati mwingine unalazimika kusitisha kufanya shughuli muhimu na za kijamii ikitokea ili kufanya ngono.
 

Iwapo mtu atapitia dalili hizi basi dhahiri kuwa mtu huyu tayari ana tatizo la kiakili na anahitaji msaada wa awali ambao ni wa ushauri kutoka kwetu wahudumu wa afya, wanasaikolojia, lakini pia kutokwa kwa viongozi wa dini kabla hali hii haijamsababishia matatizo makubwa kama vile magonjwa ya maambukizi yatokanayo na ngono na matatizo mengine ya kifamilia na kijamii.
NMG

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet